DKT.JAKAYA MRISHO KIKWETE AFUNGUA WIKI YA MAONESHO YA 3 YA UWEKEZAJI NA BIASHARA 2022
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amefungua Wiki ya maonesho ya 3 ya Uwekezaji na Biashara Mkoa wa Pwani 2022 katika Viwanja vya Mailimoja Kibaha.
Katika ufunguzi Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amesema Pwani ndio sehemu sahihi kwa sasa kwa kufanya uwekezaji sababu Dare es salaam imejaa sasa ni wakati wetu sisi wana pwani tunatakiwa kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wetu ili Mkoa wetu uzidi kukua kimaendeleo.
Aidha alibainisha kwamba,Kihistoria Mkoa wa pwani umekuwa kivuli cha Mkoa wa Dar es salaam kwa mambo mbalimbali kwa wakati ule ilikuwa unajumuisha Mkoa wa Pwani na baadae Mkoa wa Makao Makuu ya kawa hapa Kibaha.
Amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe.Abubakar Kunenge kwa kuandaa maonesho pamoja na kuweza kutenga maeneo ya kwaajili ya uwekezaji kwani kwa sasa anaona Pwani imejipanga vizuri na kwa vitendo katika sera ya uwekezaji na viwanda.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.