Waziri hiyo aliyasema hayo Leo hii wakati wa ziara ya kutembelea wilayani Mkuranga ili kuona namna ya upatikanaji wa huduma ya Nishati ya Umeme katika Kata ya Kisiju,Vikindu,Mwandege na Tambani.
Kalemani alisema"REA awamu ya pili haikufanya vizuri katika Tarafa ya Kisiju hivyo natoa siku 14 kuanzia kesho kuhakikisha umeme unawaka"
Kalemani alitoa maagizo hayo kwa viongozi wa Tanesco katika ngazi ya Mkoa na Wilaya kuhakikisha umeme huo unawaka kwa wakati.
Mbunge wa Mkuranga na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh Abdallah Ulega alisema wananchi wamekata minazi na miembe yao ili kupisha miundo mbinu ya umeme lakini ni zaidi ya miaka mitano tangu miundombinu ya umeme iwekwe na umeme haujawashwa.
Katika hatua nyingine Waziri huyo ametoa siku tano kwa mkandarasi kuhakikisha vijiji vyote vya Kata ya Vikindu vilivyopo kwenye mradi wa REA awamu ya pili vinawaka umeme.
Aidha ametoa maagizo kwa Meneja wa Tanesco Mkoa Mhandisi Martin Maduhu kumsimamisha kazi Mhandisi wa umeme bwana Dunia Ngaraba kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.
Pia amemtaka Meneja Tanesco Wilaya Mhandisi Regina Mvungi kumsimamisha fundi mchundo"Technician" bwana Frank Rwehabula kwa kushindwa kufanya kazi ya kuwasha umeme kwenye vijiji vilivyopo kwenye mradi wa REA katika Kata ya Vikindu.
"Zipo nguzo zimekaa zaidi ya miezi minne kazi haziendelei,wakandarasi eneo la mradi hawapo kabisa" Kalemani alisema
Waziri Huyo amemaliza ziara yake kwa kuwasha umeme katika Kata ya Mwandege kijiji cha mkokozi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.