Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga imejipanga kukabiliana na tatizo la lishe duni kwa kuongeza uelewa wa masuala ya lishe katika jamii, kuanzia ngazi ya familia hadi kwa watendaji na viongozi
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala Wilaya ya Mkuranga, Bi. Dalmia Mikaya kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, wakati wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti ya Lishe katika Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2020/2021, yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa mkuu wa wilaya na kushirikisha viongozi, wataalam na wadau mbalimbali wa masuala ya lishe
Aliongeza kuwa, hali ya lishe ya jamii sio ya kuridhisha, kwani takwimu zinaonesha kwa Mkuranga tatizo la upungufu wa damu kwa watoto ni 50.2%, uzito pungufu 24%, Udumavu ni 16%, Ukondefu ni 7%, huku kwa mwaka 2017 pekee 90% ya vifo vinavyotokana na uzazi vilitokana na upungufu wa damu. pia akaainisha mikakati kwa jamii ya Mkuranga kuwa ni kutoa elimu ya lishe kwa kupitia mikutano ya hadhara ya kiserikali, maonesho kwa sinema, michezo ya jadi, mashindano mbalimbali, mabango, vipeperushi n.k. na kutaka suala la lishe kuwa agenda mtambuka katika vikao vyote vya Halmashauri. Mwisho akizitaja kata zinazoongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi wa utapiamlo kuwa ni Kimanzichana, Vikindu, Mkuranga, Kisiju, Bupu, Tengelea, Njianne, Lukanga, Kiparanganda, na Mwarusembe kuwa zitapewa kipaumbele cha mradi wa kutokomeza utapiamlo.
Kwa upande wake Mwezeshaji wa Mipango na bajeti toka Ofisi ya Rais Tamisemi Bwn. Mkama Dickson Lugina, alisisitiza wadau wa masuala ya lishe kuendelea kutoa elimu ya lishe kwa jamii hususani kuzingatia umuhimu wa lishe katika siku 1000 za mtoto (tangu siku ya kutungwa kwa mimba) kuwa ndio muhimu zaidi katika kumjenga mtoto kiafya na kiakili na kumuepusha na udumavu.
Aidha alieleza mambo ya kuzingatia ili kuwa na lishe bora kuwa ni pamoja na Umuhimu wa kumnyonyesha mtoto (zaidi katika miezi 6 ya mwanzo baada ya kuzaliwa), Umuhimu wa chakula cha nyongeza, Utoaji wa vitamin A, Kupambana na ongezeka la wanawake wenye uzito mkubwa na viriba tumbo, Utumiaji wa madini joto, Makuzi changamshi na Kusisitiza umuhimu fedha za bajeti za vituo (DHFF) kupelekwa mojakwamoja kwenye vituo kwa ajili ya shughuli zenye matokeo makubwa
Naye, Afisa Lishe (M) Bi. Pamela Meena akichangia katika Mafunzo hayo ilisema, pamoja na changamoto nyingi katika kukabiliana na lishe duni, moja ya changamoto kubwa ni kutokuwepo kwa mikakati shirikishi kwa idara zote katika Halmashauri Hivyo Kuagiza kila idara kupendekeza na kuandaa Sampuli ya shughuli ambazo zitawekwa katika Mipango na bajeti za lishe katika halmashauri hiyo
Katibu Tawala Wilaya ya Mkuranga Bi. Dalmia Mikaya akihutibia wakati wa ufunuzi wa mafunzo hayo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Eng: Mshamu Munde
Mwezeshaji wa Mipango na Bajeti za Lishe kwa Halmashauri na Mkoa, Bi. Emma Vicent Kilimali akitoa maelezo katika vikundi wakati wa mafunzo hayo
Mshiriki wa mafunzo hayo akitoa mipango mikakati ya Idara mbalimbali za Halmashauri kwa ajili ya Mipango na Bajeti ya Halmashauri kwa mwaka 2020 / 2021
Mwezeshaji Mipango na Bajeti toka Ofisi ya Rais Tamisemi, Bw. Mkama Jackson Lugina akitoa mada wakati wa mafunzo
Wasiriki na wawezeshaji wa semina hiyo katika picha ya pamoja na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga
Pamela Meena, Afisa Lishe Mkoa wa Pwani akitolea ufafanuzi moja ya hoja zilizotolewa na mshiriki wa mafunzo hayo
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.