Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Bi.Mwantum Mgonja amefungua semina elekezi ya wakusanya mapato iliyofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa Halmashauri leo 27 septemba 2022.
Katika semina hiyo Bi.Mwantum Mgonja amewataka wakusanya mapato kusimamia kwa umakini mapato ili kuwezesha Halmashauri kuzidi kupata maendeleo.
Bi.Mwantum Mgonja amewataka wakusanya mapato kuhakikisha fedha zinazokusanywa zinafikishwa benki kwa wakati ili kuepuka sitofahamu ya upotevu wa fedha na endapo kuna mtu atabainika anahujumu basi hatua stahiki zitachukuliwa.
Aidha amewataka wawe na utaratibu wa kukaa wawili vituoni na kama kutakuwa na changamoto yoyote au kuona upotevu wa mapato ya Halmashauri basi watoe taarifa kwa mamlaka husika kwa haraka.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255222928730
Simu ya Mkononi: 0634329394
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2026 MkurangaDc. All rights reserved.