Kiongozi wa mbio za Mwenge Maalum wa Uhuru kitaifa Luteni Josephine Mwambashi amempa siku saba Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Ally na kumtaka kuziagiza kamati za maji zifanye marekebisho ya mwananchi kununua maji kwa ndoo shilingi 100 katika vituo vya serikali na kutaka bei hiyo ishukeLuteni Mwambashi Amesema hayo akiwa wilayani Mkuranga kukagua ujenzi wa mradi wa tanki la maji katika Kijiji cha Mkerezange na kuridhika na mradi huo uanze kufanya kazi na kutoa huduma ya maji kwa wananchi.Amesema ameridhishwa na mchakato mzima uliohusisha utekelezaji mradi huo ikiwa ni pamoja na nyaraka za matumizi ya fedha zilizotumika kwenye mradi ili mradi uanze kufanya kazi na wananchi wapate maji salamaLuteni mwambashi amesema serikali inatumia fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maji ili wananchi wapate maji safi na salama waondokane na changamoto ya kununua maji kwa gharama kubwa na kuyafuata umbari mrefuAidha pamoja na Luteni mwambashi kuridhika na mradi huo ametoa maagizo kwa mkuu wa wilaya ya mkuranga khadija Ally na kumpa siku saba kuhakikisha anashughulikia tatizo la wananchi kununua maji kwa ndoo shilingi 100‘nakuagiza mkuu wa wilaya kukaa na vikundi vya kamati ya maji, pamoja na wakala wa maji safi na usafi wa mazingira RUWASA na wananchi ili muitishe tena mkutana mjadili upya bei ya maji haiwezekana serikali inatoa fedha nyingi kutekeleza miradi ya maji halafu wananchi wanunue maji kwa bei kubwa haiwezekani naomba nipate majibu wa jambo hili mahala popoye mwenge utakapokuwa ‘aliagizaKwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga khadiji Ally amepokea maagizo hayo na kusema anashughulikia na kuyafanyia kazi maagizo yote aliyopewa na kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa na kuhakikisha bei ya maji inashuka ili wananchi wapate maji kwa gharama nafuuAidha Meneja wa wakala wa maji safi na usafi wa mazingira RUWASA Wilayani Mkuranga Maria Malale amesema mradi wa ujenzi wa tanki la maji katika kijiji cha Mkerezange pamoja na miundombinu ya usambazaji maji umegharimu shilingi milioni 984 .5Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Luteni Josephine Mwambashi pamoja na wakimbiza mwenge wenzake wamekagua miradi 15 yenye thamani ya zaidi ya shiilingi bilioni 21 ya wilaya ya mkuranga na kuridhika na utekekezaji wa miradi yote na kuizindua huku akiipongeza Mkuranga kwa kuwa na nyaraka safi za utekelezaji wa miradi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.