Msimamizi wa uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Hassani Njama amewataka viongozi wa vyama vya siasa pamoja na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wilayani Mkuranga kupitia kanuni za uchaguzi kwa umakini na kuzielewa ili kuondoa kero zisijitokeze katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Njama amesema kila aliyepewa dhamana ya kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019 ahakikishe kuwa anatimiza majukumu yake ipasavyo ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na wa haki.
Ameyasema hayo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanya cha Godown Kijiji cha Mkuranga Wilayani humo akiwa anatoa maelekezo mbali mbali yatakayofanikisha uchaguzi huo kufanyika kwa uhuru na haki na kuwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo.
Aidha akijibu maswali ya baadhi ya wananchi waliohudhuria katika Mkutano huo amesema semina zitakuwepo kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi na amewahakikishia kuwa semina hizo zitawahusisha wadau mbali mbali wa uchaguzi .
Naye Mratibu wa uchaguzi wilaya ya Mkuranga Salumu Mwamfula amewataka wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kusimamia uchaguzi kwa weledi na kuhakikisha kila hatua inafanyika pamoja na kufikisha taarifa kwa wananchi kwa wakati ikiwa ni pamoja na kubandika baadhi ya matangazo katika mbao za matangazo kama ambavyo kanuni za uchaguzi za mwaka 2019 zilivyoelekeza.
Pia amewataka wasimami wasaidizi katika ngazi zote kutoa taarifa mapema ambazo zitaashiria kuvurugika kwa uchaguzi huo.
Uchaguzi wa Serikali wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika novemba 24 mwakahuu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.