Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Mhandisi Mshamu Munde amewataka Wenyeviti wa vijiji na Watendaji wao kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuondoa changamoto za wananchi wao zilizo ndani ya uwezo wao.
Munde akizungumza kwenye kikao kazi leo aliwataka wataalamu kufanya kazi kwa kuzingatia sheria za taratibu na mwongozo kufanikisha utekelezajiilani ya uchaguzi (CCM)
Kiongozi huyo aliweka bayana kupitia mwongozo wao wa (TAMISEMI) Halmashauri hiyo inayotegemea kukusanya na kutumia mapato ya ndani sh.Bilioni 7.8 mwaka wa fedha 2022/23 inataiwa kujenga kituo cha afya na vyumba 40 vya madarasa
Mhandisi huyo alitumia fursa hiyo kuweka bayana kwa watendaji na wataalamu kufanya kazi kwa kuzingatia uadilifu huku akisisitiza kuanzia sasa suala la uhamisho kwa atakayevurunda kituo cha kazi halipo bali taratibu za kinidhamu zitachukuliwa.
Munde alisema taarifa za kampeni ukusanyaji madodoso kwa walipa kodi ya majengo zitaanza februari 5 hadi 28 na baada ya kusainiwa zitawasilishwa(TAMISEMI) mwezi machi tarehe 4,kwa mapitio kabla yah atua za utekelezaji kwenye vijiji vilivyo kwenye mpango.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.