Halmashauri ya wilaya ya mkuranga mkoa wa pwani imepongezwa kufuatia utekelezaji sera ya Taifa kivitendo kwa kuwajengea uwezo wana nchi ili waondokane na umasikini
Akifungua mafunzo kwa wajasiriamali kwenye ukumbi wa parapanda leo mkuu wa wilaya ya mkuranga fillberto sangaaliwataka wanufaika wa mkopo huo kufahamu wazi kwamba pesa hizo ni za wananchi ambazo zinztakiwa zilete tja na matokeo chanya.
Sanga aliewakilishwa na Afisa Tarafa Mkuranga anayefuatilia sera za serikali Clement Muya aliwataka wataalamu kwenye kata (25) kuhakikisha wanakua karib u na wajasiliamali kwa kutoa utaalamu ili miradi iwe na ubora.
Kiongozi huyo aliwwgiza viongozi wa vikundi kutoa taarifa kwa srikali za vijiji na wenyeviti wa vitongoji kuhusu miradi yao ili kuimarisha ufatiliaji ngazi ya kata hadi wilaya huku akiwaonya watumishi waepuke kujiunga kwenye vikundi
Awali mkuu wa idara ya aendeleo ya Jamii ,Halmashauri ya Wilaya PeterNambunga alisema wanatekeleza maagizo ya serikali kutenga asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa kuwakopesha wajasiliamali wanawake vijana na watu walemavu kwa kila mwaka wa fedha.
Nambunga alimhakikishia mkuu wa Wilaya kuwa Halmashauri imetengenea mikakati ya kuhakikisha marejesho yanawanufaisha wengine kwa kutengeneza mwongozo ambao utawabana watakaokiuka kwa kuwapelekea Mahakamani.
Akifunga mafunzo hayo yaliyowashirikisha watendaji vijiji, kata, Maafisa maendeleo ya jamiikata na wilaya, Mkurugenzi mtendaji Mhandisi Mshamu Munde alisema mikopo hiyo ambayo haina riba inalenga kuungana na azma ya serikali kufikia uchumi wa kati kwa kuhakikisha wananchi wanajiweza kiuchumi.
Munde alisema wanalenga kutoa mkopo mil (600) kupitia makusanyo ya andani bil.7.1 huku akiwataka wajasiriamali waendeleze biashara kulingana na pmbo la mradi huku akiahidi kufatilia vikundi vyote vilivyonufaika.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.