Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga imepongezwa na madiwani kufuatia hatua ya kupeleka vijijini asilimia 20 (20%) ya pesa zinazokusanywa kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato ya ndani
Akizungumza kwenye kikao maalum cha baraza la madiwani kinachopokea taarifa za utendaji kwenye kata zote (25) kilichofanyika katika hoteli ya Flex, Kiguza
Diwani wa kata ya Tengelea Shaban Manda alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri Eng. Mshamu Munde kwa maamuzi hayo.
Manda ambaye pia ni mwenyekiti kamati ya uchumi, ujenzi na mazingira aliweka bayana umuhimu wa mgao huo wa pesa katika kuchochea utekelezaji miradi ya maendeleo katika vijiji vyote (25)
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mkamba ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Afya Halmashauri hiyo Hassan Dunda aliomba zichukuliwe hatua ili kuepusha athari kufuatia kukithiri migogoro ya wafugaji na wakulima kwenye vitongoji.
Aidha madiwani mbalimbali walifikisha kilio dhidi ya ukosefu wa chakula mashuleni unapelekea utoro kwa wanafunzi sambamba na kuathiri ufaulu kiujumla.
Akimkaribisha Mwenyekiti wa Halmashauri kufunga kikao hicho Katibu ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Eng. Mshamu Munde aliweka hadharani mikakati mikakati yao ikiwemo kutoa elimu kwa Watendaji hao kuhakikisha wanaunda na kukaa kamati za ukimwi ambazo zipo kisheria .
Akifunga kikao hicho Mwenyekiti ambaye pia ni Diwani wa kata ya Magawa Juma Abeid alishukuru mahusiano mazuriya wataalam na wao madiwani hali inayofanikisha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya (CCM) na kupaisha mapato ya Halmashauri
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.