LI
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani imepongezwa kufuatia kuwa miongoni mwa Halmashauri tatu Mkoani humo kutekeleza sheria ya fedha na ilani ya uchaguzi (CCM) 2020-2025 kutenga asilimia (100) ya mapato ya ndani kwa mikopo ya vikundi vya wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu.
Akizungumza na wananchi wa mkoa wa pwani kwenye kilele cha siku ya wanawake duniani iliyofanyika Kijiji cha kimanzichana wilayani Mkuranga Mkuu wa MKoa Mhandisi Evarist Ndikilo alizitaja Hamashauri zinginekuwan ni Pamoja na Chalinze ,Kibiti
Mkuu huyo alitumia fursa hiyo kuwaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri tano zilizobaki kuhakikisha wanatekeleza aki hiyo ya msingi ili wajasiliamali wakiwemo wanawake waweze kujikwamua kiuchumi
Aidha Kiongozi huyo wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa alizitaja changamoto ambazo zinadumaza maendeleo ya wanawake kuwa ni Rushwa ya ngono mila potofu huku akitoa idadi ya wanafunzi (39) wa shule za msingi na (100) wa sekondari wamekatishwa masomo kwa mimba ndani ya Mkoa.
Awali Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii Halmashauri Mkuranga Peter Nambunga aliwataka wanawake wahamasike kugombea nafasi mbali mbali za uongozi huku wakiendelea kutoa elimu kwa wajasiliamali kuhusu kuongeza thamani ya usindikaji mazao mbali mbali
Nambunga alishangazwa amaamuzi magumu ya wanaume kutowashirikisha wanawake kwenye mipango ya maendeleo Pamoja na kuwa wamechuma Pamoja.
Naye Mhandisi Beatrice wa (RUWASA) Pwani alisema katika kutimiza malengo ya serikali awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli wametekeleza miradi sita Wilaya Mkuranga na hadi 2025watakua wamefikia asilimia(85) kwa Mkoa upatikanaji maji.
Hafla hiyo ilishuhudia utoaji wa vyeti na zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye matoke ya kidato cha nne sambamba na viongozi na wake zao akiwemo mama Ndikilo aliyeambatana na binti yake ambaye pia ni Mhandisi
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.