Mkuu wa Mkoa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ameipongeza Halmashauri ya Wilaya Mkuranga Mkoa wa Pwani kuchukua nafasi ya kumi kitaifa kwa ubora wa asali na nane kwa asali bora.
Akizungumza kwenye madhimisho ya mwaka mmoja wa programu ya “Nyuki ni fursa tuitumie” Ndikilo ambaye alituma salamu kupitia kaimu Afisa Misitu Mkoa Felix Shayo alisema Serikali ya Mkoa inatambua changamoto ya uharibifu mazingira, watumishi wachache wa sekta na vitendea kazi na kumwagiza katibu Tawala Mkoa wa Pwania asimamie upandaji miti, uhifadhi mazingira na uundaji vikundi lengo Mkoa ufikie Mikoa mingine huku akiahidi kutoa ushirikiano kutatua changamoto.
Akisoma taarifa ya Wilaya Afisa Nyuki Bi. Asted Mpita alisema wazo la Halmashauri ya Wilaya ni kuwa na kampeni ya “program ya Nyuki ni Fursa tuitumie” inachangia kuhamasisha utalii huku akiwataka wadau kutengeneza mizinga, akiongeza Afisa huyo alisema Wilaya ina mikoko ambayo ni fursa kubwa .
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Mhandisi Mshamu Munde alisema kuongezeka misitu ni ishara ya ufanisi wa kampeni hiyo.
Mhandisi huyo ambaye pia ni mfugaji nyuki alisema mazao ya chakula ni biashara pia asali ni tiba ameahidi kuungana nao kuendeleza misitu ambayo inafaida nyingi.
Akiongeza Munde alisema kampeni itaimarishwa ili itumike kuongeza mapato ya wananchi ,Halmashauri ya Wilaya na Serikali kuu kiujumla.
Akizungumza na wadau Mkuu wa Wilaya Filberto Sanga ameipongfeza Halmashauri kuandaa Hafla hiyo na kuipa kipaumbele huku akiagiza iwe endelevu hatimaye wajikomboe kiuchumi.
Sanga aliyewakilishwa na katibu Tawala Wilaya Veronica Kinyemi aliwataka waendeleze kampeni ili wananchi waelewe na kufaidika na fursa ya kujiajiri na njia zote za masoko ya uhakika.
Katika hafla hiyo Wadau mbali mbali walipewa tuzo akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri Munde ambaye ofisi ya nyuki ipo chini ya uratibu wake.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.