Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani imetekeleza sera ya fedha na ilani ya uchaguzi (CCM) mwaka 2020-25 kutoa pesa za mikopo kwa vikundi vya ujasiliamali .
Akizungumza kwenye mafunzo ya wajasiriamali ukumbi wa Parapanda leo Juni 23, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mhandisi Mshamu Munde alisema kupitia mapato ya ndani wametoa mikopo isiyo na Riba Tsh. Mil.377 kwa awamu ya tatu mwaka 2021.
Munde aliyewakilishwa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo Jamii Peter Nambunga alisema vikundi (40) vimenufaika vikiwemo wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu huku akitoa tahadhari kuwa pesa hizo sio zawadi walengwa wanatakiwa kuzirejesha kwa wakati ili wengine wakope vinginevyo sheria itafuata Mkondo.
Akizungumzia Idara yake Nambunga alisema ni mategemeo yake Uongozi wa vijiji na wataalamu wafuatilie kwa karibu maendeleo ya miradi ili baada ya marejesho wapate mikopo mikubwa na kutunisha miradi.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya Johnson Makaranga ambaye ni Afisa Tarafa ya Mkamba aliipongeza Halmashauri kwa kuboresha makusanyo ya ndani hali inayofanikisha mikopo itolewe kwa wakati na kuondoa umasikini.
Akitoa mada kwenye mafunzo hayoAfisa Uchunguzi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkuranga Hafsa Kitime aliwaonya wanasiasa wasijiingize na kuvuruga maendeleo ya vikundi hivyo huku akiweka bayana wakibainika watashtakiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya mamlaka huku wajasiriamali watakaotumia kinyume mikopo hiyo watakumbana na kosa la uchepushaji fedha.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.