WANANCHI wa vijiji vinavyounda Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani wameamua kuunda kamati za kuhamasisha na kufatilia fursa ya urasimishaji ardhi hatimaye waweze kupata hati ya umiliki iweze kuwasaidia kwenye masuala mbalimbali ikiwemo mikopo katika taasisi za fedha
Akizindua zoezi la upimaji na umilikishaji ardhi kwenye kijiji cha marogoro juzi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde aliwapongeza wananchi wa vijiji vya Mfuru mwambao,Yavayava,na Marogoro kwa mwamko wao wa kulipia Halmashauri sh.laki na nusu kila mmoja za urasimishaji huku akiviagiza vijiji vingine vichangamkie fusra hiyo ambayo imeletwa na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Raisi Dkt.John Pombe Magufuli
Munde aliwataka wananchi hao wanaozidi 100 watumie muda huu kabla septemba 29 mwaka huu ambapo wataalamu wa ardhi wataanza kupima na kumilikisha wasafishe maeneo yao, wajaze fomu maalumu yenye nakala ya malipo ya benki ili kuepuka migongano.
Kwa upande wake Afisa ardhi mteule wa Halmashauri ya Wilaya Musa Kichumu alisema wameamua kutekeleza maagizo ya Waziri wa ardhi, nyumba, na maendeleo ya makazi William Lukuvi kuwatoza wananchi hao laki na nusu huku wakizingatia kutenga barabara za mitaa maeneo ya huduma za jamii yakiwemo ya kuzikia
Naye Diwani wa kata ya vianzi yenye mradi huo Nassoro Chuma alimpongeza Mkurugenzi Munde kwa kushughulikia mapema mchakato huo wa urasimishaji kwa wananchi wake huku akiwaagiza watendaji wa vijiji vya kata hiyo wahamasishe wananchi wafaidike na mpango huo sambamba na kuwa nao bega kwa bega wataalamu wa ardhi katika upimaji na umilikishaji
Akitoa neno la shukrani katibu wa kamati ndogo ya mipango miji ambaye pia ni mnufaika Twahil Shabani “kamona” alimwomba Mkurugenzi Munde awasiliane na meneja wa (TARURA) Wilaya Mhandisi Peter Shirima ili akarabati barabara ya vikindu hadi sangatini iwe rahisi kusafirisha vifaa vya ujenzi maeneo yao.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.