Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge ametoa maagizo kwa Halmashauriya Mkuranga kuwa kabla ya June 30 mwaka huu iwe imekamilisha na kuzitolewa majibu hoja 31 zilizosalia kati ya hoja 71 kwa mwaka 2019/2020 zilizotolewa na Ofisi ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali.Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga wakati akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari kunenge kwenye kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mkuranga cha kujibu hoja 71 zilizotolewa na ofisi ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali CAG“ Alisema ofisi ya CAG katika ripoti yake iliyotolewa kwa Rais Samia Suluhu Hassani march 28 mwaka ilisema Halmashauri ya Mkuranga haikupata hati chafu lakini ilitoa maelekezo hoja 71 zilizohitaji majibu ambapo hadi sasa hoja 40 zimekwisha jibiwa na kufungwa huku hoja 31 na hoja 18 zipo nje ya uwezo wa Halmashauri‘Napenda kuwapongeza sana Halmashauri ya Mkuranga kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo yaani mmepata hati safi na pia mmetakiwa kujibu hoja 71 za CAG na hadi sasa mmejibu na kuzifunga hoja 40 bado hoja 31 kati ya hizo hoja 13 zipo ndani ya uwezo wenu hoja 18 zipo nje ya uwezo wenu ,na zilizo ndani ya uwezo wenu naagiza kabla ya june 30 mwaka huu ziwe zimefungwa zote sababu hazihitaji fedha ‘alisemaKadhalika Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani pia alitoa maelekezo kwa Halmashauri ya Mkuranga kuhakikisha wanatekeleza maagizo yake ikiwa ni pamoja na kufungwa hoja zote kabla ya ofisi ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali CAG haijaanza zoezi la kuanza kufanya ukaguzi wa mwakani unaotarajia kuanza septemba 30 mwaka huu kwa ajili ya taasisi ya bank na mahakamaAkiendelea kuzungumza katika baraza hilo kunenge aliiagiza Halmashauri kuhakikisha inaongeza bajeti katika miradi muhimu ikiwemo miundombinu ya shule hasa madarasa ambapo Halmashauri inakabiliwa na upungufu wa madarasa 1262Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde alisema wamepokea maelekezo yaliiyotolewa na Mkuu wa Mkoa pamoja na hoja zilizotolewa na ofisi ya CAG na kwamba watazifanyia kazi na kuzifunga kama ambavyo maelekezo yametolewaMunde alisema zipo changamoto ambazo zinasababisha miradi kuendelea kukwama lakini hata hivyo alisema wataongeza Juhudi ya kuzitatua changamoto zote na kuzifanyia kazi changamoto hizo na kuhakikisha miradi yote inafanya kazi.Naye Mwakilishi wa Ofisi ya CAG Mkoa wa Pwani Mary Kibogo aliipongeza Halmashauri kwa kufanya vizuri katika utekelezaji na kusimamia miradi yake ikiwa ni pamja na kufanikiwa kutoa maelezo na kufunga hoja 40 kwa weledi na alisistiza kuwa hoja zilizoanishwa zijibiwe na kufungwa mapema.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.