Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga imefanya uzinduzi wa miradi iliyoombwa na wananchi March 1,2025 katika viwanja vya shule ya Sekondari Kitumbo iliyopo kijiji cha Mkwalia Kitumbo ,Kata ya Mkuranga.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mhe.Mohamed Mwera akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg.Waziri Kombo pamoja na Wataalamu wa Halmashauri wamehudhuria uzinduzi huo.
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga imepokea kiasi cha shilingi Mil.159,453,581.58 kutoka TASAF kwa ajili ya mradi wa (TI )Targeted Infrastructure ni Mradi wa ujenzi ya miundombinu mbalimbali.
Miradi hiyo itakwenda kutekelezwa katika shule ya Sekondari Kitumbo kwa kujenga jengo la utawala pamoja na ujenzi wa madarasa mawili (2) pamoja na matundu ya vyoo sita (6) katika shule ya Msingi Malela.
Tunaendelea kuipongeza serikali ya awamu ya sita (6) inayoongozwa na Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya ya kuboresha miundombinu katika sekta mbalimbali pamoja na kuendelea kusimamia mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.