Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga imefanya uzinduzi wa zoezi la utambuzi ,usajili na ufuatiliaji wa mifugo katika kijiji cha Mkiu Kata ya Nyamato katika shamba la Mkiu Livestock Farm. Zoezi hili lipo katika sheria ya utambuzi ,usajili na ufatiliaji wa mifugo ambapo kulikuwa na uvishaji hereni kwa mifugo pamoja na uchanjaji wa chanjo ya chambafu na kimeta.
Halfa hiyo imezinduliwa na mgeni Rasmi ambae ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mhe.Mohamed S.Mwera ambae amewataka wataalamu wa mifugo kutekeleza zoezi hilo kwa kuwa linamanufaa kitaifa ambapo serikali kwa kushirikiana na wafugaji itaweza kujenga na kurekebisha miundo mbinu ya mifugo kama vile
majosho,malambo,machinjio na minada.
Mh Mwera alisema "bajeti ya Halmashauri ni finyu ila watajitahidi kuboresha na kujenga miundombinu wezeshi ya mifugo na kuwezesha upatikanaji wa vitendea kazi kwa maafisa ugani hasa pikipiki kadri bajeti itakavyoruhusu".
Wizara ya Mifugo na uvuvi kwa kushirikiana na sekta binafsi imehakikisha hereni bora za kieletroniki zinapatikana kwa wingi na kwa wakati hapa nchini. Hereni zote zitakazotumika kwenye zoezi hilo zitavalishwa nchini na zitawekwa alama maalum ya kiitroniki (barcode)ambayo itaweza kusomwa kwa kutumia kifaa maalum .Utambuzi ,usajili na ufatiliaji wa mifugo una manufaa mengi ambayo ni pamoja na kukabiliana na magonjwa ya mlipuko,hakikisho la usalama wa chakula ,kurahisisha biashara ya mifugo na mazao yake ,udhibiti wa wizi wa mifugo na upatikanaji wa mifugo iliyopotea
Wilaya ya Mkuranga imetekeleza zoezi la utambuzi ,usajili na ufatiliaji wa mifugo kwa kuzingatia mwongozo uliotolewa na Wizara ya Maendeleo ya mifugo na uvivu kwa namna moja au nyingine wanaunga mkono juhudi za serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Mkuranga Mhe.Abdallah Hamis Ulega ambaye ni Naibu Waziri katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.