Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga yaadhimisha siku ya Nyuki ni Fursa katika Kitongoji cha Mamndimpera Kata ya Bupu Wilaya ya Mkuranga.
Diwani wa Kata ya Bupu Bw.Abasi Msangule ambae ndio mgeni rasmi amewashukuru maafisa nyuki ambao wameweza kushirikiana nao vyema kwa elimu waliyotoa ya ufugaji nyuki mpaka wanakijiji wake kuweza kushiriki katika ufugaji huo ambao unaleta manufaa ki wilaya na ameishukuru Halmshauri kwa kuweza kuwapa mkopo wa shilingi laki 9,500,000/= kwajili ya kikundi cha Nyuki ni Mali.
Afisa Nyuki wa Wilaya Bi.Asted William amesema kampeni hiyo ya Nyuki ni Fursa ni endelevu na kwasasa inatimiza miaka miwili toka kuanzishwa kwake na kupiga hatua ya kuongeza uzalishaji wa asali wa mpaka Tani 9 kwa mwaka 2021 kutoka tani 1,kwa vikundi imara 25 kutoka 15 mwaka jana na pia wameweza kutoa mizinga ya kisasa 417 na Mizinga 89 ya kienyeji pamoja na mfugaji mmoja mmoja 19 na kampeni hii ni maalum kwa ajili ya kuendelea kukukumbushana mambo mbalimbali yahusuyo nyuki na fursa zake ,kujitathimini ,kutiana moyo kupongezana na mambo mengineyo.
Pia kuna changamoto ya mwamko mdogo ,hiari ya hewa kuathiri mavuno ,wizi wa asali na ghalama kubwa za vifaa vya nyuki na usafiri kwa wataalamu kuwafikia walengwa hvyo changamoto hizi kufanya kuzorotesha kwa shughuli zao kwa kiwango kikubwa sana.
Nae Kaimu DED Bi.Safina Rahim Msemo amewapongeza wana kikundi cha Nyuki ni Mali kwa uthubutu wao wa kuweza kuanzisha kikundi hicho na kuwataka kujituma zaidi ili waweze kupata mafanikio.
Maadhimisho hayo yaliweza kuzindua kwa kikundi cha NYUKI NI MALI ambacho ni kikundi cha Wanawake ambacho kina wanachama 12 ambao wamejikita kwenye miradi ya Ufugaji wa Kuku wa kienyeji, Ufugaji wa Nyuki na Kilimo cha Ufuta.
Nao wanakikundi cha Nyuki ni mali waliweza kutaja mafanikio yao waliyoweza kupata ikiwa ni pamoja mizinga 10 mipya ya kisasa ,kuwezeshwa kupata mikopo kutoka halmashauri kiasi ch Tsh.9,500,000/=,kununua mashine ya kusaga,kukoboa na kumenya nafaka na kupata mafunzo wezeshi kwaajili ya utengenezaji wa bidhaa yatokanayo na mazao ya nyuki Asali kwa kuifadhi na Jaika na kuratibiwa na Sido.
Kama kikundi kuna changamoto ambazo wanakabiliwa nazo ni pamoja na ukosefu wa umeme,ukosefu wa jengo la kuzalishia na kuifadhia bidhaa zao,ukosefu wa mashine za kuzalisha bidhaa zao ili iingie kwenye soko la ushindani na bidhaa zao kutokua au kusibitishwa na TBC.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.