Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mhandisi Evarist Ndikilo,amezitaka Halmashauri zote za Mkoa huo,kuhakikisha zinasimamia kwa uadilifu vyanzo vya mapato,ili kuleta Maendeleo kwa wananchi.
Ndikilo,aliyasema hayo hapo jana katika mkutano maalumu,wa Baraza la Madiwani,Mkuranga,uliofanyika na kujadili hoja za mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali.
Alisema kutokana na koa wa Pwani,kuwa na Halmashauri saba,amezipongeza zote kwa kupata hati safi.
Aliongeza kuwa kupatikana kwa hati safi wasibweteke na badala yake wajitume kufanya Kazi.
''Nimefurahi sana kuona Halmashauri zote saba zimefanikiwa kupata hati safi kutokana na kusimamia mapato,lakini naomba msibweteke kwa kupata hati hizo,"alisema.
Aliongeza pia kuna utaratibu ambao umewekwa na Serikali juu ya mapato ambapo Halmashauri isipokusanya mapato Kwa asilimia 80 Halmashauri inafutwa.
Alisema ni wajibu wa kila Halmashauri kuhakikisha inasimamia vizuri mapato yake ili isije ikavunjwa kwa kushindwa kufikia asilimia 80.
Aliongeza kuwa, ili kuendelea kufanya vizuri Halmashauri inatakiwa vyanzo vya mapato lazima vifanyiwe utafiti mzuri ili viweze kuwasaidia katika ukusanywaji wa mapato.
Alisema ni jukumu la wataalamu kuhakikisha wanasimamia vizuri vyanzo vya mapato ili vilete maboresho katika Halmashauri.
Aliongeza kuwa mapato yakusanywe vizuri na yasiishie katika mifuko ya watendaji wasio waadilifu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.