Shirika la ‘Hope for Young Girls’ la Kinondoni jijini Dar es saam limetoa jumla ya baiskeli 25 kwa wanafunzi wa kike wanaosoma katika mazingira magumu ya umbali kulinganisha na shule ilipo ndani ya wilaya ya Mkuranga
Shirika hilo linalojishughulisha na utoaji elimu kwa mabinti ili waweze kujitambua na kufahamu haki zao kielimu na kijamii hususani mapambano dhidi ya mimba za utotoni, limetoa msaada huo kwa shule tano wilayani hapa ambazo ni Tambani, Tengelea, Isima, Mpugilo na Magawa
Akiongea na Mkuranga DC wakati wa kukabidhi baiskeli hizo, kiongozi wa shirika hilo Bi. Salama Kibudu alisema msaada huo umekuja baada ya kuona mabinti wengi wanaotoka mazingira magumu wanapata changamoto kufika shule kwa wakati na wengine kupata vishawishi wawapo njiani na kupelekea mimba za utotoni hali inayokwamisha jitihada za kumkomboa mtoto wa kike kielimu
Akipokea msaaada huo kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Mkuranga, Afisa Tarafa ya Mkuranga Ndg. Clement Muya alisema msaada huo umekuja wakati muafaka ambapo wilaya inapambana kutafuta muarobaini wa kuboresha viwango vya ufaulu;
“Leo nimefurahi sana kwa jambo hili ambalo ni jipya kabisa tangu nimekuja hapa Mkuranga na litasaidia sana kwani ukiangalia mazingira yetu ya shule za kata nyingi zipo ‘scatted’ hivyo baiskeli hizi zitawasaidia sana wanafunzi hawa”
Kwa upande wa wanufaika wa msaada huo, Najma Hassan mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Tambani alishukuru kwa msaada huo na kuahidi kuongeza bidii katika masomo , Huku Bi. Khadija Salum ambaye ni miongoni mwa wazazi waliohudhulia tukio hilo alipongeza jitahada hizo na kuwataka wanafunzi hao kuweka juhudi katika masomo na kuachana na mambo ya anasa
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.