Mkuu wa idara ya Elimu sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Mwl. Benjamin Majoya leo amezungumza na Afisa Habari Wilaya kuhusiana na maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha sita ambao wanatarajiwa kuripoti shuleni kuanzia tarehe 1/6/2020
Mwalimu Majoya alisema wao kama idara kwa ushirikiano wa walimu wa shule zote zenye kidato cha sita ambazo ni shule ya sekondari Mwinyi, Nasibugani na St Mathew walijipanga mapema kwa kuwasaidia wanafunzi na kuwaandalia masomo na kuwatumia kwa njia ya mtandao ili waweze kujisomea wakati walipokua wanasubiri tamko la Serikali.
Sambamba na hilo Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari alisema “hawa watoto walishasoma na tayari walikua wameshajiandaa kwa ajili ya mitihani yao ya mwisho kilichotokea baada ya tamko la kufungwa kwa shule kiliwahuzunisha na kuwapunguza morali lakini anaamini wanafunzi wa kidato cha sita ni watoto wenye uelewa ukilinganisha na wale waliopo madarasa ya chini…
Akizungumzia changamoto ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na kirusi cha corona alisema wao kama walimu wamejipanga kusambaza ndoo za maji na sabuni katika shule zote na kuwasisitiza wazazi wanapowarejesha watoto mashuleni mapema mwishoni mwa wiki hii wasisahau kuwapa barakoa nyingi kadri ya matumizi ili waweze kujilinda wakiwa maeneo ya Shule
Kwa kuhitimisha bwana Benjamini alisisitiza atashirikiana na Idara ya Afya ya Hamashauri ya Wilaya kwa kuwaomba waende kutoa elimu zaidi mashuleni kwa kipindi ambacho watoto hao watakapokua wanasubiri kufanya mtihani wa kumaliza kidato cha sita ila kuwaongezea elimu zaidi kuhusiana na mapambano ya kirusi cha Corona
Mitihani ya kidato cha sita inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka huu kama tamko la serikali lilivyosisitiza chini ya Wizara ya Elimu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.