Kamati ya Ukaguzi ya TAMISEMI ikiongozwa na Bw.Sigsbert Valentine Kaijage wamekagua miradi iliyotolewa fedha na serikali kuu kwenye miamala ya Tozo pamoja na fedha za Uviko 19 ambapo halmashauri ikiwa msimamizi mkuu wa miradi .
Kamati hiyo imeridhishwa na miradi hiyo na kumpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Bi.Mwantum Mgonja pamoja na Wataalam wote kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo ya maendeleo.
Pia Bw.Sigsbert Valentine Kaijage ambae ni Mkurugenzi ofisi ya Rais TAMISEMI amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga kuhakikisha miradi ambayo bado haijakamilika basi wasimamie na ikamilike kwa muda uliopangwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.