Kamata ya Ulinzi na usalama ya Wilaya ya Mkuranga imepokea mrejesho wa mafunzo elekezi ya kufatilia bidhaa za afya (Health Commodities Tracking ) katika mnyororo wa ugavi wa vituo vya kutolea huduma za Afya.
Mafunzo hayo amabao yaliandaliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI iliandaa na kufanya mafunzo kwa Team ya RHMT na CMHT ili kuwajenga uwezo wa kufanya ufatiliajia wa bidhaa za afya (Medicine Audit/Tracking) ikijumuisha ufatiliajia wa mwenendo wa ununuzi ,utunzaji na matumizi ya dawa ,vifaa na vifaa tiba na vitendanishi.
Aidha Mwenyekiti wa kamati ya Usalama ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe.Hadija Nasri Ali amependekeza katika ukaguzi wa robo mwaka au wakaida vituoni waende kwa Pamoja na kamati ya Usalama ili na wao waweze kupata uelewa wakujua ni kwa namna gani wataweza kushirikiana kwani jukumu lao kwa wananchi kupata huduma nzuri kwani huwa ni jambo zuri kwao .
Nae Daktari Ael Mende ambae ni Mfamasia wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga amesema serikali ya Tanzania ili kuhakikisha Afya ya wananchi wake inakuwa salama ,imedhamiria upatikanaji wa bidhaa za Afya zenye ubora ,salama na bei nafuu kwa 100% jambo linaloakisi kwa kiasi kikubwa ubora wa huduma zitolewazo katika kituo husika .Licha ya juhudi za serikali kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa za Afya unakuwa kwa aslimia 100% bado kumekuwa na changamoto za usimamizi wa bidhaa katika vituo vya kutolea huduma za Afya .
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.