Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Bi. Zuwena Omari amefanya ziara ya kutembelea Miradi ya Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Kisegese na Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Msorwa.
Akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Bi. Mwantum Mgonja, Katibu Tawala ameweza kujionea Miradi hiyo ambapo amepongeza usimamizi wa miradi hiyo na kupongeza kamati za ujenzi pamoja na wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga.
Bi.Zuwena Omari amesisitiza miradi hiyo kuendelea kusimamiwa kikamilifu ili iweze kukamilika kwa wakati. Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Pwani pia amepata Muda wa kuzungumza na watumishi katika ukumbi wa Flexi Garden Kiguza na kuwakumbusha kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma kwa Watumishi wote wa Halmashauri hiyo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.