Kaya zaidi ya 100 Wilayani Mkuranga zimeathirika na mvua katika vijiji vya Makumbea na Magawa katika kata ya Magawa Wilayani Mkuranga.
Akizungumza na wananchi wa vijiji vilivyoathirika hapo jana,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mh.Juma Abeid aliwafariji waathirika wa mvua hizo kwa kuwapa chakula yaani unga na maharage kwa lengo la kuwasidia kwa kipindi hiki cha maafa.
Abeid aliongeza kwamba kuna watu wengine wamepoteza maisha kutokana na mvua hivyo ni vema sasa wananchi wakajihadhari na mvua zinazoendelea kwani zinaweza kusababisha madhara makubwa zaidi.
“Ni vema kuwakataza watoto wasitoke endapo kunaonekana kuna madhara ambayo yanaweza kusababisha watoto wetu kupoteza maisha kwani mpaka sasa tayari kuna vifo vimetokea kwenye baadhi ya maeneo”Juma Abeid alisema
Bi zedi Bakari Mkazi wa Magawa anasema”Mvua zimeniathiri kwa kiasi kikubwa na maji yanatokea chini kama chemchem hivyo kwa sasa sina mahala pa kulala,kuku wangu wote 20 wamekufa na vifaa vyangu vingine vimeharibika kama mikeka,ukili na nguo”
Wakati huo huo watu watatu wamethibitika kufariki kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuzama kwenye mto wakati wakiogelea na wengine kufariki kutokana na kuvuka mto.
Waliothibitika kufariki ni Sumaiya Jumanne mwenye umri wa miaka(3) jinsia ya kike ambae alizama kwenye mto wakati anaogelea kwenye mto wa Kinungamkele uliyopo katika kijiji cha kiziko kata ya mwarusembe,Said Athumani mwenye umri wa miaka (7) jinsia ya kiume,darasa la kwanza katika shule ya Msingi Vianzi iiyopo Wilayani Mkuranga,alifariki kutokana na kuzama kwenye bwawa lililopo karibu na shule ya sekondari Vianzi,na Mwingine ni Faruha Twaha mwenye umri wa miaka (5) jinsia ya kike,darasa la awali katika shule ya Msingi Majimatitu ambaye alizama wakati akivuka kutoka Majimatitu kwenda kitongoji cha Churwi kijiji cha Mlamleni Kata ya Tambani Wilayani Mkuranga.
Aidha Mwili mmoja wa Kauthar Twaha ambae ni dada wa Faruha Twaha bado haujapatikana ambae walikuwa pamoja na dada yake wakivuka kutoka Majimatitu kwenda Churwi na juhudi za kumtafuta zinaendelea.
Kauthar Twaha ni Mwanafunzi wa kike darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Churwi mwenye umri wa miaka 7.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.