Siku ya maadhimisho ya miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu iliyofanyika kwenye kituo cha mikutano wa Julius Nyerere,Dar es salaam.
Halmashauri ya Wilaya Mkuranga tulipata nafasi ya kupeleka mmoja wa watoto wa walengwa wa TASAF kutoka kijiji cha Mwarusembe ambae kwa sasa yupo chuo kikuu cha UDOM na amepata mkopo asilimia 100% baada ya kutambuliwa kama mtoto ambae ametoka kwenye kaya za walengwa wa TASAF.
Kijana Iddi Kawambwa ametoa ushuhuda mbele ya Waziri Mkuu Mhe.Kasimu Majaliwa namna alivyoweza kumudu gharama za ada na chakula baada ya kufanikiwa kupata mkopo 100% uliofanikisha kwenda chuo kikuu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.