Kituo cha Afya Mkamba Wilayani Mkuranga kimefikia hatua ya mwisho za ujenzi wa miundombinu ambapo ujenzi huo umeelekezwa kwenye chumba cha upasuaji,wodi ya wazazi,Maabara na Nyumba ya Mganga.
Mwenyekiti wa kamati ya Afya kituo cha Afya Mkamba bwana Haji Abdallah alisema ujenzi ulianza mwanzoni mwa mwezi machi ambapo walipokea kiasi cha Tshs milioni 400 kwa ajili ya ujenzi huo ambapo fedha zilipokelewa mwishoni mwa mwezi Disemba 2017.
Bwana Abdallah aliongeza kwamba baada ya kupokea fedha hizo waliendelea na maandalizi ya awali ikiwemo usafishaji wa eneo linalotarajiwa kujengwa na pia kusubiri ramani mpya kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwakua walipata taarifa juu ya ramani mpya ambazo zitatumika kwenye vituo vya Afya.
Aidha Bwana Abdallah aliendelea kusema kwamba ujenzi umefika kwenye hatua mbalimbali ambapo nyumba ya Mganga na Maabara zipo kwenye hatua ya umaliziaji na wodi ya wazazi pamoja na chumba cha upasuaji ziko kwenye hatua ya upauaji.
Bwana Bakari Mpili mjumbe wa kamati ya manunuzi alisema wamefanikiwa kununua baadhi ya vifaa kwa bei rahisi kutoka viwandani ambapo vifaa walivyonunua viwandani ni mabati na misumari na vifaa vingine wamenunua dukani kwa bei za kuridhisha kulingana na soko lilivyo.
Mwenyekiti kamati ya ujenzi bwana Hamisi Omari Mwidoe alisema ujenzi unaendelea vizuri ila kulikuwa na changamoto ya ucheleweshwaji wa vifaa kutokufika kwa wakati ambapo zaidi ilikuwa kwenye kokoto, mawe na mchanga kutokana na hali ya hewa ambapo sehemu wanapochukua vifaa hivyo kulikuwa kumejaa maji.
Kamati ya ujenzi imeadhamiria kuhakikisha ifikapo mwishoni mwa mwezi Aprili ujenzi huo utakuwa umekamilika ambapo kutakua na chumba cha upasuaji, wodi ya wazazi,maabara na nyumba ya mganga.
Kituo cha Afya Mkamba baada ya kukamilika kitasaidia kupunguza umbali wa huduma za upasuaji kwa wananchi na pia kituo hiki kinatarajiwa kuwahudumia wananchi wa kata mbalimbali kama kisegese, Panzuo, Nyamato, Kimanzichana, Mwarusembe, Lukanga na Magawa.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.