Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amewahakikishia wakulima wa korosho Mkoa wa pwani kwamba msimu wa korosho 2023-2024 amejipanga kuhakikisha wakulima wote wanapata haki zao pindi mauzo yatakapoanza na kuhakikisha wanawachukulia hatua kali kwa wote wataokwamisha wakulima wa korosho Mkoa wa Pwani.
Kunenge ameyasema hayo alipofungua mkutano wa wadau wa korosho Mkoa wa pwani ambao umefanyika oktoba 5 katika ukumbi wa Flex Garden Kiguza Mkuranga.
Katika Mkutano huo Kunenge alimpongeza Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuondoa changamoto za wakulima sambamba na kuwatumikia Watanzania kwa lengo la kuboresha maisha yao.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nasri Ali amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea wakulima wa Mkuranga pembejeo za kutosha na madawa kwaajili ya kilimo.
Akifafanua Mkuu wa Wilaya, aliweka bayana asilimia (70) za Pembejeo zote Mkoa wa Pwani zimekuja Wilaya ya Mkuranga huku akimhakikishia Mkuu wa Mkoa kusimamia kwa weledi na umakini mkubwa mauzo ya Korosho kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.
Aidha kiongozi huyo alisema kutokana na tahadhari ya mvua maghala yatafunguliwa kwenye Amcos tarehe 10 mwezi oktoba na mnada wa kwanza utafanyika tarehe 25 Oktoba 2023.
Akiwasilisha salamu za Wabunge wa Mkoa wa Pwani , Mbunge wa jimbo la kibiti Abdallah Mpembenue alimpongeza Rais Dkt. samia kwa kuhamasisha masuala ya kilimo na Viwanda huku wakiahidi kumpa ushirikiano kusimamia zao la Korosho ambalo kwa kiasi kikubwa linagusa wananchi.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Chama cha ushirika Mkoa wa Pwani (CORECU) Hamisi Mantalewa ameweka bayana kuwa wanazidi kuboresha Miundombinu ambayo itakuwa rafiki kwa wakulima wa korosho ambapo wameanza kugawa vifungashio kwa baadhi ya AMCOS pamoja na vipima unyevu ambavyo vitasaidia kupata korosho zilizo bora na kuwahakikishia wakulima kwamba watapata malipo yao kwa baada ya siku 10 .
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.