Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge ameipongeza wilaya ya Mkuranga kwa kuandaa sherehe za Kimkoa maadhimisho ya wiki ya msaada kisheria.
Kunenge aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Hadija Nasri amezipongeza Asasi za msaada wa kisheria na wananchi ambao wameweka kando itikadi huku akiziagiza Halmashauri zote za Mkoa wa Pwani kutenga bajeti ambayo itafanikisha wananchi kupata msaada wa kisheria.
Mkuu wa Wilaya amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri Mwantumu Mgonja kutenga jumamosi ya mwisho wa mwezi kusikiliza msaada wa kisheria.
Naye Afisa Ustawi wa Jamii kiongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani Widman Masika Alipongeza uwepo wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria kupitia kauli mbiu “Mtoto Kwanza” wametoa mafunzo vijiji (108) na kata (25) wamezindua Baraza la wazee Wilaya na kupata wawakilishi wawili kwenye koa wa Pwani.
Masika alifika mbali zaidi kwa kuwasaidia watu wenye ulemavu kupata mikopo ya Halmashauriya wilaya sh. Mil.77 na kuandaa mafunzo kwa waendeshaji vituo vya chekechea.
Masika alisema wametoa vyeti vya kuzaliwa elfu 46,821, Bima ya afya wametoa kwa kaya 1326 na kupokea hukumu ya kifungio cha Maisha moja na kifungo miaka (30) sita ameomba elimu itolewe kwenye nyumba za ibada na kutaja changamoto bajeti ndogo na wananchi hawana uelewa
Akitoa neno la shukrani Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Mohamedi Mwela aliupongeza uongozi wa mkoa kwa uenyeji wa sherehe hizo huku akiahidi kuwatumia Madiwani wenzake na wataalamu chini ya Mkurugenzi Mwantumu kutekeeza maagizo ya Mkuu wa Mkoa.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.