MKURANGA YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA
Hatimaye ile siku adhimu ya kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika leo imekamilika baada ya viongozi na wananchi mbalimbali ndani ya Wilaya ya Mkuranga kushiriki siku hiyo katika kituo cha SARAH HOUSE kilichopo Kijiji cha Mwandege.
Katika kuadhimisha siku hii, watoto walipata fursa ya kuonesha vipaji mbalimbali kwa kuonesha stadi zao za kazi, kucheza, kuimba sambamba na kuonesha umuhimu wa mtoto kupata kwa njia ya maigizo.
Akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nassir Ali, Afisa Tarafa ya Mkuranga Clement Muya amesema kila Mzazi au Mlezi ana wajibu wa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kusimamia na kuhakikisha watoto wanapata elimu safi kwani tayari Mh, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kuimarisha, kuboresha na kuongeza majengo mapya katika Sekta hiyo.
Awali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Waziri Kombo amewaasa watoto wote kuacha matendo ya hovyo na badala yake wasimame imara katika kushika elimu ili waweze kufikia malengo yao.
Maadhimisho hayo Mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu isemayo, "Elimu jumuishi tuzingatie maarifa, maadili na stadi za kazi"
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.