Akiwahutubia wananchi waliojitokeza katika viwanja vya wazi katika kijiji cha Kisemvule, Mh. Mkuu wa Wilaya Filberto Sanga alisema kuwa maambukizi ya Ugonjwa wa UKIMWI katika wailaya ni asilimia 4.3 (4.3%) aidha maambukizi makubwa yako kwa wanawake kwa asilimia 3.9 (3.9%) na wanaume asilimia 1.6 (1.6%).
Alizitaja baadhi ya tabia zinazochangia kuwepo kwa maambukizi mapya kuwa ni :-
1. Mila na Desturi Mbaya kama vile mikesha ya ngoma za Usiku na kurithi wajane bila ya kupima VVU
2. Ulevi wa kupindukia
3. Ngono bila ya kutumia Kinga (Kondom)
4. Wajawazito wenye VVU kujifungulia nyumbani bila kuchukua tahadhari. Alitoa wito kwa mama wajawazito kuzingatia tarehe zao za makisio na kusogea karibu na zahanati au hospitali ya wilaya ili waweze kupatiwa huduma bora na hivyo kuzuia maambukizi mapya kwa watoto wanaozaliwa.
5. Utumiaji wa madawa ya kulevya.
6. Kuwepo kwa hospitali za vichochoroni au majumbani ambapo matibabu yanafanyika bila kuratibiwa kwa kutumia vifaa visivyo salama.
Mwisho alisisitiza juu ya kufikiwa kwa asilimia 90 ya wananchi kufahamu Afya zao, Asilimia nyingine 90 ya Usajili kwenye Vituo vya Matunzo na Tiba na asilimia nyingine 90 ya walioathirika kuendelea kupata dawa ili ifikapo 2020 maambukizi mapya ya VVU yasiwepo kwani UKIMWI unaathari kubwa kwa Uchumi wa Familia na Taifa kwa Ujumla.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.