Takwimu za maambukizi ya virusi vya ukimwi zimeshuka kutoka asilimi 4.9 hadi kufikia asilimia 3 kuanzia January 2020 hadi kufikia Desemba 2021
Hayo yamesemwa leo katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Mkuranga.
Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Bi Hadija Nasri Ali alisema kwa kipindi cha Januari hadi Octoba 2021 jumla ya watu 28,125 wamejitokeza kupima Virusi vya Ukimwi ambapo wanaume ni 12,280 na wanawake 15,845 waliobainika kuwa na maambukizi ni 879 kati ya hao wanawake 556 na wanaume 310 hivyo kufanya wilaya kuwa na maambukizi ya asilimia 3.
Ametaja magonjwa makuu yasiyoambukiza ni pamoja na mishipa ya damu, saratani, kisukari na magonjwa sugu yasababishayo kuziba mfumo wa upumuaji
Akiwasilisha taarifa ya magonjwa yasiyoambukiza Mtaalam wa afya Bi Juliana Mpwata alisema takribani watu milioni (36) kila mwaka huathirika na magonjwa yasiyoambukiza sawa na asilimia 80 na watu mil (29) hufariki kutokana na magonjwa hayo haswa katika nchi za vipato vidogo na vya kati, aliendelea kusema magonjwa ya moyo na mishipa ya damu ndio sababu ya vifo vingi vya watu mil. 17 ikifuatiwa na kansa mil. 7, mfumo wa upumuaji mil. 4 na kisukari milioni 1.
Akihitimisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Bi, Mwantumu Mgonja alimhakikishia mkuu wa Wilaya kuwa maelekezo yote akiyoyatoa watayafanyia kazi hususani katika swala la mazoezi ili kuufanya mwili kuwa imara na afya bora.
Maadhimisho hayo yalipambwa na kauli mbiu isemayo "kauli mbiu ya tokomeza ukimwi, tokomeza magonjwa yasiyoambukiza"
Takribani jumla ya watu 28125 wakiwemomwake kwa waume , hayo ameyasw,a ,eo Mkuu wa wilaya Mkuranga Mhe. Hadija Nasri
Zingatia usawa tokomeza ukimwi,tokomeza magonjwa ya mlipuko

Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.