Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ya Mkuranga Rehema Mwakibuja Tarehe 12 septemba 2024 amefanya kikao na Wajumbe wa Baraza la Kata katika viwanja vya soko la Zamani Vikindu.
Katika kikao hicho Mwakibunja amesema mabaraza ya Ardhi ya Kata yana mamlaka ya kutoa huduma ya kusikiliza, kushauri na kutatua migogoro yote ya Ardhi katika Kata zao.
Amesema Kama mwananchi hajaridhika na maamuzi ya kisheria yanayotolewa na mabaraza ya nyumba ya Wilaya ana haki ya kukata rufaa kwenda mahakama kuu na kama ana malalamiko ya kiutendaji na nidhamu basi malalamiko hayo yapelekwe kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi ili yafanyiwe kazi.
Nae Clement Muya Afisa Tarafa ya Mkuranga amesema Wilaya inawategemea sana Wajumbe wa Mabaraza ya Kata katika kupunguza migogoro ya Ardhi kwa wananchi kwani majukumu waliyonayo ni makubwa katika jamii hivyo amehusia tutumie vyeo walivyokuwa navyo kwa kufata haki, sheria na kanuni zilizowekwa.
Aidha wamejionea zoezi la Kliniki ya Ardhi linavyoendelea katika viwanja hvyo na Kumpongeza Mkuu wa idara ya Ardhi na Mipango miji Bw.Said Swalehe pamoja wasaidizi wake kwa kazi wanayofanya kupitia Kliniki hii ya Ardhi na wameomba liwe zoezi endelevu na kuzifikia mpaka Kata za Vijijini.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.