Naibu Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula awaagiza wakurugenzi wote Nchini kuwasimamia wataalamu wa rdhi ili waendeshe zoezi la kurathimisha Ardhi vijijini hatimaye wananchi wapate hati zitakazowawezesha watumie ardhi yao kwa dhamana ili kupata mikopo katika taasisi mbali mbali za fedha ili wajikwamue kiuchumi
Mabula Ameyasema hayo wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Mkuranga Mkoa wa Pwani akimuagiza Afisa Ardhi Mteule Mussa Kichumu kuhakikisha anawaogoza wataalamu wenzake kufuatilia mashamba pori yenye hati miliki katika vijiji vyote 125 na kuwapa notisi kisha wawasilishe kwake vielelezo tayari kwa kuyabadilishia mpango.
Aidha Mabula alimtaka Afisa Ardhi Mteule Wilaya ya Mkuranga awape notisi ya mahakama wadaiwa sugu wote walipe tozo za serikali sambamba na kuingiza kwenye mfumo viwanja vyote na mashamba ili kuboresha ukusanyaji wa mapato ndani ya Wilaya
Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mathew Nhonge alihitimisha mgogoro sugu wa wakazi wa Kikoo na Miale kwa kukabidhi Ramani yenye viwanja 334 huku akiahidi kuwaongoza wataalamu wake kwenye migogoro ya kiwilaya ili kufafanua tafsiri ya mipaka.
Aidha Mabula alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde kuandaa na kupeleka andiko kwake ili waweze kupatiwa mkopo utakaofanikisha kupima maeneo mbalimbali huku wakizuia ujenzi unaoendelea wa makazi holela
Akitoa neno la shukrani Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga alimhakikishia Naibu Waziri kusimamia maagizo yote likiwemo la kuyawezesha Mabaraza ya Ardhi ili yatembelee kwenye migogoro hatimaye haki ipatikane mapema na kukomesha dalili zozote zinazoashiria vitendo vya rushwa
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.