Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Ndg Filberto Sanga leo ametoa agizo kwa vyombo vya ulinzi na usalama la kufunga madanguro yote yaliyopo ndani ya Wilaya ya Mkuranga kwa lengo la kuendelea kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi ambayo kiwilaya wameweza kuvuka lengo kwa asilimia 94 tofauti na matarajio ya Wilaya ambapo lengo lilikua ni asilimia 90.
Akizungumza katika Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Dunia yenye kauli mbiu, Sanga alisisitiza kwa kusema Madanguro ni lazima yafungwe kwa sababu lengo la uanzishwaji wa madanguro hayo sio mzuri Zaidi unalenga kuendelea kusababisha maambukizi ya ukimwi kwa watu wapya.
Akitoa angalizo juu ya matendo ya ulawiti Sanga aliwataka wazazi kujenga utamaduni wa kuwakagua Watoto mara kwa mara na kufatilia kwa karibu mienendo na michezo wanayocheza na Watoto wengine hii pia itasaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi hasa kwa Watoto wenye tabia za kulawiti Watoto wenzao.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde alitoa pongezi za dhati kwa taasisi zisizo za kiserikali kwa kushirikiana na iIdara ya Afya na uongozi wa Wilaya kwa ujumla kwa kuendelea kusaidia watu wenye mahitaji maalumu ikiwemo kutoa vifaa vya shule na kadi za bima ya afya CHIF kwa kaya 896 zilizopo mkuranga na taasisi isiyo ya kiserikali ya JIMOWACO
Maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yalisindikizwa kwa kauli mbiu isemayo “MSHIKAMANO WA KIMATAIFA , TUWAJIBIKE KWA PAMOJA ILI KUTOKOMEZA JANGA LA UKIMWI”
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.