Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani imepanga kutumia Shilingi Milioni 200 kwa ajili ya ununuzi wa Gari la Mkurugenzi.
Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha Robo ya kwanza 2022/2023 kwenye ukumbi wa Flex Garden Kiguza Mkuranga jana, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ndg, Mwantum Mgonja amesema tayari wamepata baraka za Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ili kuendelea na mchakato huo.
Katika kikao hiko Madiwani kwa sauti moja wamempongeza Mh Rais Samia Suluhu Hassan kwa kubuni na kukusanya mapato ya tozo ambayo kwa kiasi kikubwa zimefungua miundombinu ya mwasiliano Mijini na vijijini.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Barabara Mwaka 2022/2023 Kaimu Meneja wa TARULA Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Bernard Mwita amesema amepokea Shilingi Bilioni 2, ambapo bilioni 1.5 za Mfuko wa Maendeleo na Milioni 500 za Mfuko wa Jimbo.
Aidha alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe.Samia Suluhu Hassan kuwaletea fedha hizo ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa kutengeneza Barabara na Madaraja.
Akitoa salam za Serikali Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe.Khadija Nasri Ally amewapongeza Madiwani na Wataalam wakiongozwa na Mkurugenzi kwa ushirikiano wao ambao umechangia kuboresha mapato ya Halmashauri na kuwataka wasimamie matumizi na ubora wa Miradi ya Maendeleo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.