Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga leo Agosti 15 imefanya ziara ya ukaguzi wa eneo linalotarajiwa kujengwa zahanati lililopo Miale kata ya Mkuranga kwa lengo la kujiridhisha mipaka na uhalali wa eneo hilo kabla ya kuanza kwa ujenzi.
Mbali na eneo hilo, kamati pia ilifanya ukaguzi kwenye maeneo mbali mbali kwa lengo la kuangalia athari za kimazingira zinazoweza kuathiri afya ya Wananchi kwenye maeneo husika.
Maeneo yaliyotembelewa ni pamoja na eneo linalochimbwa madini ya udongo unaotumika kutengeneza vigae, kiwanda cha Saruji cha Diamond sambamba na kiwanda cha bingwa kinachotengeneza bidhaa za kufanyia usafi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255222928730
Simu ya Mkononi: 0634329394
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2026 MkurangaDc. All rights reserved.