Madiwani wanaounda Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani wamepitisha bajeti ya Halmashauri yenye jumla ya sh. Bil. 49.7 zikiwemo bilioni 7.8 zinazotarajiwa kukusanywa kupitia mapato ya ndani ili kutekeleza miradi ya maendeleo sekta mbali mbali kwa mwaka 2021-22
Akitoa taarifa kwenye kikao hicho maalum leo 18/2/2020 Afisa Mipango wa Halmshauri ya Wilaya Bi Kaunga Amani alitaja vipaumbele vya bajeti hiyo ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi (CCM) ya mwaka 2020-25 sera ya Nchi na maelekezo ya Serikali kupitia Waziri wa (TAMISEMI) Selemani Jafo.
Akichangia kwenye Baraza hilo Diwani wa Kata ya Dondwe Abduli zombe alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mhandisi Mshamu Munde ameahidi kusimamia vyanzo vipya vya mapato hususani kwenye fukwe za kisiju, kwale na palacha ambavyo vina historia kubwa katika Nchi
Akitoa salamu Mbunge wa jimbo la Mkuranga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari ,Sanaa, utamaduni na michezo Abdallah Ulega aliwapongeza Madiwani kwa kuibua hoja za kuendeleza mapato kutokana na fukwe zilizopo katika Halmashauri hiyo huku akiahidi kutumia vikao vya juu kuboresha barabara ikiwemo ya kutoka Kisiju hadi Mkuranga na Vikindu hadi Vianzi
Akifunga kikao Mwenyekiti wa Halmashauri Mohamed Mwela aliwataka wataalamu wasimamie ubora wa miradi ya maendeleo huku akiweka wazi kuwa mkali Kwenye makusanyo hatimae wananchi wafaidike na maendeleo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.