Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga limepitisha Bajeti ya Tarura kwa Matengenezo ya Barabara Mwaka wa Fedha 2022/2023 na mapendekezo ya Bajeti mpya kwa mwaka wa Fedha 2023/2024.
Bajeti hiyo ilipitishwa sawa na maoni ya wadau mbalimbali yaliyotolewa kikaoni hapo ambapo jumla ya kiasi cha shilingi 1,064,830,000.00 kiliidhinishwa na hadi sasa utekelezaji upo katika hatua mbalimbali.
Baraza hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa flex Garden Kiguza na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nassir Ali, Mbunge wa Jimbo la Mkuranga ambae pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Abdallaha Ulega na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga Veronika Kinyemi.
Wengine ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga Mwantum Mgonja na Wakuu wa Idara na vitengo mbalimbali wa Halmashauri hiyo pamoja na wananchi.
Akitoa tamko la Serikali Mkuu wa wilaya ya Mkuranga ameshauri kila Robo mwaka Halmashauri itenge Fedha kwa ajili ya kuweka taa za Barabarani ili kuwe na fursa ya usalama wa raia na hata kwa wafanya biashara kwa nyakati za usiku.
Aidha amemtaka Mkuu wa Idara ya ardhi kutekeleza Mpango wa mipango Miji sambamba na upimaji wa ardhi wakati tarura wanapambana na kutengeneza Barabara ili kuepuka Migogoro ya ardhi ya mara kwa mara.
Nae Mbunge wa jimbo la Mkuranga Ambae pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi amempongeza Mh. Rais wa awamu ya sita Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza Bajeti ya Barabara Mkuranga Kutoka Milioni 800 mwaka 2018 hadi kufikia Shilingi Bilioni 1,000,000,000 kwa sasa.
Akitoa ufafanuzi wa asilimia 10 ya fedha zinazotokana na mapato ya ndani kwenda Tarura Mkurugenzi amewataka Madiwani kuwa na subila kwani tayari kiasi cha shilingi Milioni 600 kimetengwa kwa ajili ya Barabara.
Akifunga Mkutano wa Baraza hilo Mwenyekiti wa Baraza hilo Mohamed Mwela amewataka Tarura kusimamia vema nidhamu ya Bajeti iliyopangwa ili kufanikisha ujenzi wa Barabara za Mkuranga zinakuwa na viwango vinavyohitajika.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.