• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
    • TASKSMIS |
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Rasimali watu na Utawala
      • Industrial, Trade and Investment
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Mipango,Sera na Takwimu
      • Ardhi na Maliasilli
      • Maji
      • Ujenzi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mazingira na Usafi
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Mawasiliano Serikalini
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Mipango na Uongozi
      • Elimu, Afya na Maji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Sera
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Photo Galley
    • Habari Mpya
    • Matukio

MADIWANI MKURANGA WAPITISHA TAARIFA YA MAENDELEO ROBO YA TATU

Posted on: April 29th, 2025

Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani limepitisha taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha.

Akizungumza katika kikao cha baraza hilo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga, Mohamed Mwela, alisema madiwani wamepitisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mujibu wa bajeti ya mwaka 2024/2025, ambapo zaidi ya shilingi bilioni 14 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo, zikigawanywa katika robo nne kupitia mapato ya ndani.

Aidha, Mwela alisema kuwa pamoja na ajenda ya miradi ya maendeleo, kikao hicho pia kilitumika kutoa elimu kwa madiwani kuhusu umuhimu wa bima ya afya kwa wote.

"Tumepata elimu, hii elimu tutaitumia kuwafikishia wananchi ili wajue umuhimu wa bima ya afya kwa wote," alisema.

Akizungumzia mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita, Mwela alisema kuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ni kipenzi cha watu wa Mkoa wa Pwani, wakiwemo wananchi wa Mkuranga, kutokana na namna serikali yake inavyowaletea maendeleo kupitia miradi mbalimbali mikubwa.

Alisema kupitia serikali hiyo, Mkuranga imenufaika na mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni tano unaotekelezwa eneo la Mkwalia, ambao unahudumia wakazi wa Kata ya Mkuranga pamoja na vijiji vya jirani.

Vilevile, alisema Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga imeboreshwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 900 kupitia bajeti ya mwaka 2023/2024.

Kwa upande wa sekta ya elimu, Mwela alibainisha kuwa halmashauri hiyo imefanikiwa kupata zaidi ya shilingi bilioni 4 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya ufundi katika Kata ya Mkamba, Kijiji cha Kizapara.

Aliongeza kuwa pia wamefanikiwa kupata mradi wa maji kwa vijiji saba katika halmashauri hiyo, sambamba na uboreshaji mkubwa wa miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari, akisema:

"Pongezi kubwa zimfikie Rais Samia kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Mkuranga. Shukurani zetu kwa Mama Samia tutazionyesha Oktoba mwaka huu katika Uchaguzi Mkuu," alisema Mwela.

Aidha, alitumia nafasi hiyo kutoa pongezi kwa Mbunge wa Jimbo hilo, Abdallah Ulega, kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi cha 2015 hadi 2025.

Matangazo

  • TANGAZO LA VITUO VYA USAILI January 21, 2025
  • ORODHA YA MAJINA YA WAANDISHI NA WAENDESHA VIFAA January 21, 2025
  • Tazama vyote

Habari Mpya

  • SILAA AELEKEZA TCRA KUFIKA RADDY FIBER MKURANGA

    June 18, 2025
  • RC KUNENGE AIPONGEZA MKURANGA KUPATA HATI SAFI

    June 17, 2025
  • UWT YAZINDUA KAMPENI YA UTOAJI ELIMU ILANI YA CCM

    June 11, 2025
  • PROFESA NAGU APONGEZA HUDUMA ZA MAABARA MKURANGA

    June 05, 2025
  • Tazama vyote

Video

SIMAMIENI MAADILI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Fomu ya Ruhusa ya Ugonjwa kwa Watumishi (Sick Sheet Form)
  • FFARS user manual
  • Matokeo ya Darasa la Saba 2020
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • uchaguzi wa wanafunzi kujiunga kidato cha kwanza 2020/2021 Mkuranga
  • Barua pepe za ofisi za watumishi
  • Fomu ya Likizo kwa Watumishi
  • Fomu ya Ruhusa kwa Watumishi
  • Fomu ya Maombi ya Leseni ya Biashara

Tovuti Linganifu

  • TAMISEMI
  • e-GA
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Ajira
  • Ikulu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Baraza la Mitihani la Tanzania
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
  • Mkuranga Tasks Management Information System (Tasks MIS)

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Visitors Counter

Free Visitor&Stat Counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga

    Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania

    Telephone: +255232110038

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma zetu

Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.