Wajumbe wa kamati ya uchumi, ujenzi, na mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani imempongeza mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mhandisi Mshamu Munde kufuatia ubunifu wa vyanzo vya mapato
Akizungumza kwenye kituo cha mabasi kiguza baada ya kutembelea uboreshaji wa kituo hicho, Mwenyekiti wa kamati hiyo Shabani Manda ambaye pia Diwani wa kata ya Tengelea alimtaka Mhandisi wa ujenzi Shahidu Mudrica kuhakikisha gharama za mradi zinaendana na ubora halisi.
Kwa upande wake mjumbe wa kamati hiyo Fatma Shally anayeongoza kata ya Mbezi (viti maalumu) alimwagiza mhandisi wa ujenzi ahakikishe mradi huo unaisha mapema ili Halmashauri iboreshe mapato sambamba na wananchi wafaidike kuuza biashara mbali mbali kwenye soko jirani na kituo cha mabasi
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255222928730
Simu ya Mkononi: 0634329394
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2026 MkurangaDc. All rights reserved.