Madiwani Mkuranga wanaounda Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani wametaka kuwepo kikao cha wadau wa korosho kabla ya usambazaji pembejeo ili kudhibiti ubora wake.
Akifungua kikao cha Baraza cha kupokea taarifa za utekelezaji kwenye kata kwa robo ya tatu Januari-Machi 2020/2021 Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mohamed Mwella alisema zao la korosho ni tegemeo kwa uchumi wa wananchi na Halmashauri kwa ujumla hivyo kabla ya kugawa dawa kwa wakulima watajiridhisha ubora wake.
Aidha mwella ambaye pia Diwani wa Kata ya Mkuranga aliwataka Madiwani wenzake kuorodhesha barabara mbovu za kipaumbele ili wakabidhiwe wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Mkuranga ili kutatua changamoto za mawasiliano vijijini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ambaye pia ni Katibu wa kikao Mhandisi Mshamu Munde aliwageukia watendaji kata zote (25) na kuwaambia wawe makini katika uaandaji wa taarifa zao ikiwemo mapato na matumizi na kuziwasilisha ofisini kwake kwa wakati.
Akiwasilisha taarifa ya kata ya Dondo Diwani Abdul Zombe alitaka Halmashauri kuipa kipaumbele kata hiyo ambayo amezaliwa Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi kama alivyoeleza kwenye kitabu chake alichozindua hivi karibuni.
Naye Diwani wa Kata ya Tengelea Shabani Manda aliungana na mwenzake Zombe kwa Wilaya hiyo kutoa Rais Mstaafu huku akiomba Halmashuri kuangailia upya msaada aliopanga kusaidia Hospitali ya Wilaya Mwanaye Asma Mwinyi ambao utaboresha utoaji huduma za afya.
Kabla ya kufungwa kikao hicho Mkurugenzi Munde alipongeza Madiwani kuwavumilia Watendaji katika uwasilishaji taarifa za utekelezaji zilizo kamili .
Kikao hicho kilifungwa kwa Mwenyekiti Mwela akiwataka Madiwani wenzake kuwabana Wataalamu wao watekeleze maagizo ambayo ni sehemu ya kanuni za Halmashauri ya Wilaya.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.