Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani waliokutana leo kwenye ukumbi wa Flexi kiguza wameupongeza mpango mpya wa Serikali kuwashirikisha kwenye utekelezaji wa Miradi ya barabara.Akiwaongoza wenzake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mohamed Mwella alimpongeza mwalikwa Mratibu wa (TARURA) Mkoa wa Pwani Mhandisi Lutifyo Mwakigonja kwa ufafanuzi wake ambao umerejesha mahusiano mazurina (TARURA) Wilaya.Akiwasilisha mpango huo mpya Mratibu mkoa Muhandisi Mwakigonja aliweka bayana Bunge wameboresha Muundo kuanzia Mwaka ujao wa fedha kutakua na barqza maalumu la madiwani ambalo wataWashirikisha Wataalamu wa (TARURA) Wilaya kujadili changamoto za barabara Mjini na VijijiniKatika kikao hicho Kamati za Kudumu za huduma za Halmashauri ya Wilaya waliwasilisha taarifa zao ambazo Diwani wa kata ya Tengelea Shabani Manda aliiomba Halmashauri kuajiri Wataalam wa Xray ili kufanikisha utolewaji huduma hiyo nyeti kwa wagonjwa.Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Elimu na afya ambaye pia Diwani wa kata Mkamba Hassani Dunda ameagiza Vituo vyote vya afya na Zahanati Wilayani humo kuorodheshwa Wataalam waliopo ili kuangalia kwa kina maboresho kwenye sekta ya afya.Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri Mhandisi Mshamu Munde amewaahidi Madiwani kuendelea kuboresha maeneo mbali mbali ili kuleta tija katika kuqaletea maendeleo wananchi kama Ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyojieleza.Akifunga kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri Mohamedi Mwera aliwaomba Madiwani wapta na waliorejea tena kujenga ushirikiano hatimaye wananchi waboreke kimaendeleo
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.