Baraza la Madiwani Wilayani Mkuranga wameuomba uongozi wa Wakala wa barabara mijini na vijijini (TARURA- Tanzania Rural and Urban Roads Agency) kutoa elimu kwa waheshimiwa madiwani kwa lengo la kuelewa jinsi inavyofanya kazi kwa mustakabali wa wilaya ya Mkuranga.
Waheshimiwa hao waliyasema hapo jana wakati wa mkutano wa kawaida wa baraza la madiwani wa kujadili taarifa za robo ya kwanza katika ukumbi wa kiguza flex(Tibaigana) hapo jana.
Mh Edward Kowero Diwani wa kata ya Mwandege alihoji juu ya utendaji kazi wa TARURA kwa kuwa haitakuwa chini ya uangalizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga hivyo haitakuwa na ufanisi wa kutosha hususan wananchi wana mategemeo makubwa kuhusu upatikanaji wa miundombinu ya barabara iliyo bora katika ngazi ya mjini na vijijini.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mh.Juma Abeid alitoa ufafanuzi juu ya jambo hilo kwa kusema ”kuna vyombo vingi vya serikali ambavyo vinafanya kazi na Halmashauri lakini haviko chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri lakini vinafanya kazi vizuri kabisa hivyo tuondoe hofu”
Aidha Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Bwana Salum Papen alisema TARURA ipo kisheria na imepitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo Baraza la madiwani halina mamlaka ya kukataa utendaji kazi wa TARURA.
Wakati huo huo, Baraza la madiwani walitaka kupata mrejesho juu ya nyumba za watumishi ambapo kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani uliopita wa tarehe 13/09/2017 iliazimia hatua za kisheria zichululiwe na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga kupitia vyombo vyake vya kisheria ikiwemo TAKUKURU na Polisi dhidi ya watumishi waliohusika na hatua zote za ujenzi wa nyumba za watumishi.
Baraza la Madiwani lilisema kwakua Mkuu wa Wilaya ndio alikuwa anashughulikia jambo hili ni vema mrejesho upatikane kutoka kwake, hivyo baraza limeazimia kikao kijacho cha mkutano wa Baraza la madiwani wapate mrejesho juu ya hatma ya nyumba za watumishi na watumishi wote waliohusika.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.