Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga imetoa mafunzo kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu vinavyotarajiwa kupata mkopo kipindi cha Robo ya Tatu Mwaka wa Fedha 2024-2025.
Mafunzo hayo yamefunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Mohamed Maundu na yamefanyika katika ukumbi wa Mwinyi Sekondari hapo Mei 20,2025 na yatadumu kwa muda wa siku 3.
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga kupitia mfuko wa Maendeleo ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu imekuwa ikitoa mikopo ili kuwawezesha na kujikwamua kiuchumi,mikopo hii inayotolewa kwa mujibu wa sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa Sura 290 kifungu cha 37A kinaelekeza juu ya utoaji na Usimamizi wa mikopo ya 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri.
Kwa Kipindi cha Mwaka wa Fedha 2024-2025 Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga imetenga kiasi cha Tsh.1,181,921,900 kutoka katika Makusanyo ya 10% ya mapato ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo .
Aidha kufikia Mei,2025 Halmashauri imekwisha toa mikopo yenye jumla ya Tsh 976,278,250 kwa vikundi 53 ambapo vikundi vya wanawake 18 vimepata Tsh.201,433,000,vikundi vya vijana 28 vimepata Tsh.696,828,250 na vya watu wenye ulemavu 7 kiasi cha Tsh.78,017,000 na Mikopo hii imetolewa kwa awamu 3 na utoaji wa mikopo bado unaendelea.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.