Asasi ya Umoja wa Shirika la Vijana Mwandege(USHIVIMWA) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga imeendesha mafunzo ya siku tatu katika ukumbi wa parapanda kwa wasichana 90 kutoka katika kata za Mkuranga,Vikindu na Mwandege.Mafunzo hayo ni mwendelezo ya mafunzo kama hayo yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana kwa wasichana 150 walioko shuleni katika kata za Mkuranga,Vikindu na Mwandege.Wasichana 90 ni wale walio nje ya shule walipatiwa mafunzo mbalimbali ikiwemo stadi za maisha,madhara ya dawa za kulevya,madhara ya mimba za utotoni na ujasiriamali kwa vitendo.Wasichana hao walijifunza kwa vitendo namna ya ufugaji wa kuku wa asili na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali kwa kutumia muhogo na unga wa muhogo.
Afisa Maendeleo ya Jamii kitengo cha Vijana Bi safina Msemo kwa niaba ya Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya alisema kwamba lengo la mafunzo haya ni kuwafanya wasichana kujikomboa na hali ngumu ya maisha pia kuepuka kuwa tegemezi jambo linaloweza kusababisha kujiingiza kwenye vitendo vya ngono zembe ili kujipatia kipato na hatimae kupata magonjwa ya zinaa pamoja na VVU/UKIMWI na kupata mimba zisizotarajiwa.
MKurugenzi wa USHIVIMWA bwana Mohamed Mbonde alisema"baada ya kutafakari kwa kina juu ya adha zinazowakabili wasichana wengi ndani ya jamii illiyopo mtaani na kubaki kuwa kama watumwa ndani ya jamii zao kutokana na kutojihusisha na shughuli za kujiingizia kipato inyotokana na ukosefu wa elimu ya ujasiriamali ndipo tulipoamua kutoa mafunzo kwa vijana hao", Bwana Mbonde aliendelea kusisitiza kwamba vijana hao wanatakiwa kuwa na mawazo ya biashara kabla ya kufikiri namna ya kupata mtaji.
Meneja wa Mradi Nuri Kiswamba alisema mafunzo hayo ni katika utekelezaji wa mradi wao uliofadhiliwa na Taasisi ya The Foundation For Civil Society ambapo umegharimu Tshs mil 50. Aliendelea kusema kwamba mradi huu ulianza tangu octoba 2016 na unatarajia kumalizika mwishoni mwa mwaka huu.Aidha alisema mradi huu ulijikita katika katika nyanja mbalimbali hasa za Elimu juu ya uzazi,athari za matumizi ya dawa za kulevya na ujasiriamali.
Akifuga mafunzo hayo yaliyodumu kwa siku tatu Afisa Maendeleo ya Jamii kitengo cha vijana Bi Safina Msemo alizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Idara hiyo alisema ni wakati muafaka kwa vijana hasa wanawake kujitokeza na kujikita katika ujasirimali kutumia fursa ili kujikomboa na umaskini wa kipato hasa ukizingatia mkakati wa Serikali wa kuifikia Uchumi wa kati wa Viwanda.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.