Mafunzo kwa vikundi vinavyotarajiwa kupewa Mkopo wa 10% ya vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu yamehitimishwa leo Novemba 11,2024 katika ukumbi wa uthibiti ubora katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga.
Mafunzo hayo yametolewa kwa siku 3 ambayo yanaratibiwa na idara ya maendeleo ya Jamii yenye lengo la kuwaelimisha juu ya usimamizi na uendeshaji miradi yenye tija ili waweze kurejesha fedha za mikopo waliyopewa.
Mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii Bi.Mwanamsiu Dossi amefunga mafunzo hayo na kuwataka wawezeshwaji kuhakikisha wanafata taratibu zote zilizowekwa katika mikataba waliyopewa na kuhakikisha mikopo waliyopewa inarejeshwa kwa wakati.
"Kupitia mafunzo haya mmefundishwa mbinu mbalimbali za kuendesha vikundi hivyo basi muyafanyie kazi na mnapokwama Maafisa Maendele Jamii Kata wapo kwa ajili yenu kuhakikisha mnafikia malengo mliojiwekea kwani mikopo hii ipo kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi".
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga imetenga kiasi cha shilingi Bil.2,133,795,818.92 kwa Mwaka wa fedha 2024/2025 kwa ajili ya kukopesha vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.