Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mh Juma Abeid amemkabidhi gari la wagonjwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mkuranga leo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo yaliyofanyika kwenye hospitali ya wilaya ya Mkuranga.
Akitoa ufafanuzi Mh Juma Abeid alisema kwamba tangu hospitali ya wilaya kuanzishwa Halmashauri haijawahi kununua gari la wagonjwa kutokana na mapato ya Halmashauri lakini kwa sasa mapato yaliyopatikana yamesaidia kununua gari la wagonjwa ambapo imegharimu mil 137.
Mh juma Abeid aliongeza kuwa “Tumeanza na gari la wagonjwa na baadae tunatarajia tununue X-Ray kwani tumeomba muda mrefu kununuliwa lakini mpaka leo bado hatujapata kwakua uwezo wa kukusanya tunao tutatumia mapato yetu ya ndani ili kupunguza kero mbalimbali kwa wananchi wetu”
Mweyekiti wa kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira Mh Nicholaus Kampa alisema kwamba kumekuwa na shida sana ya gari la wagonjwa Mkuranga lakini baada ya kufanya vikao vya maamuzi tukaona ni vema mapato yetu yakatumika kununua gari la wagonjwa kwani tupo hapa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wetu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde baada ya kukabidhiwa gari la wagonjwa na Mwenyekiti wa Halmashauri alisema atahakikisha gari la wagonjwa linatumika ipasavyo na kutunzwa vizuri ili liwasaidie wananchi wetu.
Sikudhani Juma ambaye alikuwa shuhuda wakati wa makabidhiano ya gari la wagonjwa alisema anashukuru Halmashauri na viongozi wake kwa jitihada iliyofanya kupata gari la wagonjwa kwani litasaidia kupunguza vifo visivyo vya lazima hasa kwa wakina mama na watoto.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.