Wazazi na walezi wa wanafunzi wanaosoma kwenye shule za msingi na sekondari Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani wametakiwa kujenga utamaduni wa kuchangia chakula ili kuboresha ushiriki wa watoto wao sambamba na kupaisha kiwango cha ufaulu
Akifungua mkutano wa marafiki wa elimu Wilayani humo uliofanyika kwenye ukumbi wa parapanda Mkuranga jana Afisa elimu sekondari wa Halmashauri ya Wilaya Benjamini Majohe alipongeza asasi ya kiwalani inayoongozwa na Rehema Ngelekele kwa kusimamia utafiti kwenye shule (19) uliolenga kuibua changamoto zinazowakabili watoto wa kike .
Aidha aliwahakikishia wanafunzi wa kike na wazazi kiujumla kuwa Halmashauri ya wilaya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali watahakikisha wanawakomboa kwenye changamoto hizo kuu za ukosefu wa chakula ,mila na desturi kandamizi miundo mbinu kwa watoto wenye ulemavu na kujenga uzio mashuleni.
Nao marafiki wa elimu walichangia changamoto za utafiti kwa kuziomba Mamlaka husika zisimamie wazazi wapewe elimu ya jinsia na watoto wa kike wachezwe unyago baada ya elimu ya msingi sambamba na Halmashauri ya Wilaya itunge sheria ndogo itakayowabana kwenye vibali wa vigodoro walinde mmomonyoko wa maadili hususani kwa watoto wa kike wenye umri mdogo
Kivutio kikubwa kilikuwa shairi lenye beti kumi lililosomhawa kwa kichwa na mwanafunzi wa kike darasa la saba anayesoma shule ya msingi Mponga,Tatu Hamisi aliyetoa ushuhuda wa umuhimu wa kumuelimisha mtoto wa kike akiwataja viongozi akiwemo makamu wa Raisi Bi. Samia Suluhu Hassani huku akiwapongeza shirika la Haki Elimu kwa kuwezesha utafiti na mkutano
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.