Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani lililokutana kujadili taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi robo ya pili Octoba hadi Desemba 2020 imeazimia kujenga matundu ya vyoo kwenye shule za sekondari Marogoro na NK,wyamato ili kuhakikisha wanafunzi wanaanza masomo.
Akizungumza kwenye kikao hicho Katibu wa kikao ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mhandisi Msamu Munde alisema amefanya maamuzi hayo ili kuwaokoa Watoto kutembea umbali mrefu ili kupata masomo .
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Dondo Abdul Zombe Pamoja na kupongeza ubunifu wa Mkuu wa Wilaya kutatua changamoto ya sekta ya elimu kwa kuanzisha kiwanda kidogo cha kutengenezea madawati katika viunga vya ofisi yake lakini amemwomba kupanua karakana hizo ambazo pia ajira kwa vijana zipanuliwe hadi ngazi ya Tarafa na kata ili kuongeza kasi.
Akitoa neno la shukrani Diwani wa kata ya Nyamato Faraji Kisebengo alisema kutokana na changamoto kubwa Watoto wa Nyamato kutembea kilometa (15) kufuata shule Mkiu ilibidi achangie shilingi laki tatu ili kufanikisha shule hiyo muhimu.
Madiwani wamemuomba Mkurugenzi Munde afuatilie kwa karibu Wizara ya Ardhi nyumba maendeleo ya makazi ili watekeleze agizo la Rais Dkt John Magufuli kuwapa wananchi wa vijiji vya Luzando na Magodani maeneo ambayo tayari wataalamu wa ardhi Halmashauri wamepanga matumizi
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.