MBUNGE WA JIMBO LA MKURANGA AIPONGEZA WILAYA YA MKURANGA KWA KUWEKA MAOTEO YA MAENDELEO.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga ambae pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla Ulega ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani kwa kuweka maoteo ya makusanyo yenye bil.(9) hali itakayochangia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Akizungumza kwenye Baraza la Madiwani la Bajeti mwaka 2022/2023 kwenye ukumbi wa Flexi Kiguza Mhe.Ulega ameipongeza Halmashauri hiyo kutenga sh.milioni(348) kwaajili ya kupima ardhi ili kuongeza thamani .
Aidha aliweka bayana uthamini wa ardhi utawaokoa wafugaji na wakulima ambao watanufaika kwa kupata haki itakayowezesha kukopa benki.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.